2020 ulikuwa mwaka usioweza kusahaulika, uliojaa zawadi na changamoto zisizotarajiwa. Wakati dunia ilikabiliana na janga la COVID-19, timu za Life In Abundance katika nchi 14 barani Afrika na Karibea ziliendelea kufanya yale ambayo tumekuwa tukifanya siku zote: kuyawezesha makanisa na viongozi wa jumuiya kukidhi mahitaji ya wale walio karibu nao. Kwa kufanya hivyo, na kutafakari juu ya uaminifu wa Mungu katika yote hayo, tunajua kwamba 2020 ilileta ukuzi na hekima mpya.






